|
Zenjydar Community Association H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE È 07886 535282
|
|
|
Community Airlines ni shirika jipya la ndege la binafsi ambalo huduma zake linahudumu abiria ndani nchi (Tanzania), na mpaka sasa huduma zake ni nzuri na hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa abiria wake.
Community Airlines, Air Tanzania na Uganda Airlines
Ofisi ya Community Airlines iliyopo Dar es salaam International Airport
Khalid Said Salim Bakhresa (pichani) amefariki dunia baada ya kupata ajali akiwa kwenye mashindano yaliyofanyika Zanzibar sehemu za Kiwengwa Inasemekana gari la marehemu lilipinduka akiwa ankwepa watoto barabarani. Marehemu alizikwa huko huko Zanzibar katika mazishi yaliyohudhuriwa na mamia ya waombolezaji akiwemo rais wa Zanzibar, Mh. Amani Abeid Karume na viongozi wengine kadhaa. Mungu amuweke mahala pema peponi. Amin.
Ndugu, jamaa na marafiki walikuja kumzika marehemu Khalid
Baba yake marehemu Khalid (Salim) akionekana na uso wa majonzi
Baadhi ya waendeshaji magari ya mashindano walikuja kumzika mwenzao
Gari ya marehemu ambayo aliyokuwa akishindania nayo kabla ya ajali
Gari ya marehemu baada ya ajali
Gari ya marehemu baada ya ajali
Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na waimbaji maarufu wa marekani BOYZ II MEN ambao alikutana nao katika mkutano uliofanyika Washington DC, wa kuleta maendeleo ya Afrika.
Timu ya taifa ya Zanzibar maarufu kama Zanzibar Heroes, imeaga mashindano ya chalenji ya Cecafa, kishujaa, kwa kufungwa mabao 5-4 na Rwanda kwa njia ya penalti baada ya kutoka 0-0 katika dakika 90. Mshambuliaji wa taifa stars, Abdi Kassim ndiye aliyekosa penalti na kuua kabisa matumaini ya bongo kuingia nusu fainali na hatimaye fainali na kunyakua ubingwa.
Salam kutoka kwa Mheshimiwa Balozi Mwanaidi Sinare Maajar katika Kusherehekea Sikukuu ya Eid-El-Hajj, Noeli Na Mwaka Mpya 2008
Ndugu Watanzania
wenzangu na wote wenye mapenzi na nchi yetu mlioko hapa
Uingereza na Jamhuri ya Ireland. Kwa niaba ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa niaba ya wafanyakazi wenzangu katika Ubalozi wa Tanzania London, na kwa niaba yangu binafsi napenda kushirikiana nanyi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kufikia kipindi hiki muhimu. Katika kipindi cha mwaka mmoja Ubalozi wenu umekuwa ukijitahidi kuwajibika kibalozi na kushirikiana kwa namna mbalimbali na Watanzania walio katika eneo letu la uwakilishi. Katika kipindi hiki pia tumejitahidi kupigania kuimarisha mshikamano wa Watanzania na hatimaye kufanikiwa kuunda upya Jumuiya ya Watanzania baada ya kuwa kimya kwa muda. Ni matumaini yetu kuwa Watanzania watailinda na kuiinua Jumuiya yao kwa mafanikio yao na Taifa letu kwa ujumla. Watanzania tuna sifa kubwa ya kuheshimiana, kuvumiliana na kushikamana bila kujali itikadi zetu za kisiasa, imani zetu za dini au kabila au rangi. Ni matumaini yetu tutaendelea kudumisha mshikamano wetu siku zote tukifanya kazi kwa bidii ili tuchume ugenini na kuweza kuijenga nchi yetu. Katika kusherehekea sikukuu hizi muhimu natumaini tutakuwa na fursa nzuri ya kutembeleana na kuimarisha mshikamano kati yetu. Nawapeni nyote mkono wa Eid El Hadji, mkono wa sikukuu ya Noeli na kuwatakia kheri ya Mwaka Mpya ujao. Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania. Balozi, Mwanaidi Maajar
Waislamu wa East London walikutana katika sala ya Eid-el-hajj iliyofanyika Manor Park katika jengo la Ravadassia Community Centre. Pichani juu ni Ustadh Khamis akitoa hutuba ya Eid.
Maalim Seif Sharif Hamad aliungana na waislam wengine waliofika katika sala ya Eid-el-hajj, East London.
Kutoka kushoto chini ni Ustadh Khalfan, Ustadh Hafidh, Maalim Abdallah, Maalim Seif na Ustadh Nassor
Ali Muhidin wa Tanzaniaone akipeana mkono na maalim Seif
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijumuika na waumini wenzie kusali sala ya Eid-el-hajj katika msikiti wa BAKWATA, Kinondoni Muslim asubuhi leo. bada ya sala pia alihutubia baraza la iddi lililofanyika hapo hapo msikitini.
Pantoni ya MV Alina ikitokea kigamboni ikiwa imebeba abiria na magari huku ikikaribia kutua nanga nchi kavu
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali hivi karibuni Ikulu, kutathmini miaka miwili tangu serikali yake ilipoingia madarakani, Desemba mwaka juzi. Rais Kikwete katika mazungumzo yake na waandishi wa habari aligusia mambo mbalimbali likiwemo suala zima la utendaji wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO), kwamba limekuwa na utendaji wa kusua sua, hivyo serikali inakamilisha muswada wa mabadiliko ya sheria ya nishati kwa lengo la kuruhusu kampuni binafsi kuzalisha na kusambaza umeme ili kuleta ushindani kwa shirika hilo na kuleta huduma bora kwa wananchi.
Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bwana Mbarak M. Abdul-wakil, Ikulu mjini Dar es salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Philemoni Luhanjo na Katibu wa Baraza la Mawaziri Bw. Mkwizu.
Rais wa awamu ya pili ya Tanzania, Alhajj Ali Hassan Mwinyi akiwa na waziri wa habari, utamaduni na michezo mh. Muhammad Seif Khatibu, na profesa Amandina Lihamba ambaye ni naibu mwenyekiti wa bodi ya magazeti ya serikali akila pozi katika kuadhimisha mwaka mmoja wa gazeti la (Habari Leo). Wakwanza kulia ni kaka Issa Muhidin Michuzi.
Cheka na vikatuni
Usiangalie unene wako, angalia uzito wako... - Tutumie picha na habari tofauti za kutoka popote na tutaziweka kwenye mtandao - Email: zenjydar@gmail.com - - Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran! |
|
|
|