Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

22/12/2007

USALAMA

Usalama wa jiji ulitayarishwa mapema kupambana na yoyote yatakayotokea ambayo yatakayohatarisha usalama wa raia katika kipindi cha Eid-el-hajj, Krismas na mwaka mpya 2007.

MAALIM SEIF NA WANACHAMA WA CUF

Maalim Seif alikutana na wanachama wa CUF katika hotuba yake aliyeitoa akiwepo mjini Northhampton UK, na kujibu maswali yaliyoulizwa juu ya msimamo wa CUF na CCM.


23/12/2007

EID-EL-HAJJ FESTIVAL 2007

Eid-el-hajj festival 2007, iliandaliwa na Zenjydar Community Association, ikiwa kama ni moja ya siku kuu ya kusheherekea kisa cha nabii Ibrahim (a.s) na mtoto wake Ismail (a.s). Katika tamasha hilo kuliandaliwa na michezo tofauti ikiwamo michezo ya kuigiza ya kiislamu kama ionekanavyo hapo juu pichani. Kisa cha hapo juu ni ustadh Omar Salim akiwaambia wanafunzi wake umuhimu kuhusu sala na kuwafundisha maadili mazuri ya kuwafanya wao waepukane na matendo mabaya kama magenge, madawa ya kulevya, n.k.

Ikiwa kama ni mara yetu ya kwanza kuandaa tamasha la Eid, tumefurahi baada ya tamasha kuisha kupokea email na mawazo tofauti kwa njia ya simu kutoka kwa watu tofauti. Na tumeyapokea mawazo yao na vilevile tutayatumia katika tamasha lijalo mwakani. Inshallah.

Ilikuwa ni siku ya furaha kwa watoto na familia nzima

East African Education Foundation na Alnoor Cultural & Education, pia walishiriki katika kuunga mkono fikra ya tamasha hiyo na vilevile jumuiya iliyofika hapo iliwaunga mkono katika kuongeza mfuko wa vyama hivyo. Ilikuwa ni siku ya furaha kwa kila mtu.

Kulia ni Ustadh Hafidh wa EAEF, Ustadh Masoud wa Alnoor, Ustadh Sabry wa Alnoor, Ustadh Said wa Alnoor.

Familia zilizofika wakiwa na watoto wao katika tamasha la Eid-el-hajj

Watoto wakiwa katika 'bouncy castle'

Zawadi zilitolewa kwenye steji baada ya maswali na majibu kwa watoto


24/12/2007

DAR ES SALAAM YAZIDI KUSHAMIRI

Majumba ya vioo yazidi kuzagaa mjini Dar

KAZI NI KAZI

Safari ya maili mia...


25/12/2007

SANAMU LA BISMINI

Sanamu la bismini lililopo Dar es salaam, limekutwa limefunikwa na mfuko wa plastik kwenye uso wake na kiroba chake cha mgongoni. Ni nani aliyefanya kazi hiyo? Na kamaanisha nini?


26/12/2007

SHATI

Shati kubwa kuliko yote Tanzania, lililopo katika duka moja mjini Dar es salaam, limewekwa kwa kutolewa bure ikiwa kuna mtu litakayemtosha.


27/12/2007

MSIMU

Msimu wa matunda hasa mananasi umeanza. Mia tano umekula asali

BENAZIR BHUTTO AUWAWA

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Benazir Bhutto amefariki dunia katika mji wa Rawalpindi, Pakistan, baada ya mtu aliyesimama karibu na gari lake kujiripua na bomu na kusababisha watu 20 kuuwawa na kujeruhi baadhi ya watu. Miji mingi ya Pakistan ilivurugika kwa ghasia za wananchi kutokana na kifo cha Benazir Bhutto. Habari zaidi bonyeza hapa.


28/12/2007

UNGUJA

Unguja ilivyo sasa kwa juu

KATUNI

Cheka na vikatuni

HII SIO KATUNI


- Tutumie picha na habari tofauti za kutoka popote na tutaziweka kwenye mtandao - Email: zenjydar@gmail.com -

- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk