Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

03/11/2007

WANJA LA MPIRA

TRENI-GARI

GARI-TRENI

Mambo hayo hapo juu yapo India


04/11/2007

INJINI KIUNO

Unaweza kukadiria bei ya baiskeli hii? na hali ya kuwa unajua injini kiuno?

PANCHA

Ama kweli akili haihitaji nguvu!


05/11/2007

MISS TANZANIA - 2007

Miss Tanzania 2007, Richa Adhia ameshatua China. Akionekana pichani na Miss Trinidad & Tobago 2007, Valene Mahalaj. Fainali ya Miss World 2007 itakuwa siku ya Jumamosi tarehe 1 Disemba 2007.

MVUA YA MAWE - KIGOMA

Kigoma walibahatika kupata mvua ya mawe tunavyoiita nyumbani, ambayo huku ulaya wanaita "sleet".


06/11/2007

GATI JIPYA - ZANZIBAR

Juu pichani ni daraja jipya la gati, Zanzibar

FORODHANI - ZANZIBAR

Washabik wa Liverpool Zanzibar wakiwa na Issa Michuzi wakishangilia ushindi wa Liverpool kwa kuifunga Besiktas magoli 8-0.

DARAJANI - ZANZIBAR

Pichani juu ni eneo la Darajani, Zanzibar. Kwa wanaojua nyumbani watakwambia namba hiyo inakwenda wapi

Boda kwa boda


07/11/2007

AIRPORT - ZANZIBAR

Pichani juu ni lonji ya kupumzikia abiria kabla ya kupaa na ndege

AJALI HAINA KINGA

Ama kweli ajali haina kinga. Hapo juu ni mitaa ya Dar es salaam

MEXICO YAPATA DHORUBA

Baada ya mafuriko makubwa yaliyoipata mji wa Villahermosa, Mexico, karibu maelfu ya watu wameachwa bila ya makazi na malaji. Asilimia themanini (80%) ya mji wa Tabasco umezamishwa kwa maji na kuuwa watu na mifugo kama ng'ombe waonekanavyo kwenye picha ya hapo juu. Villahermosa kwa lugha ya kispanish maana yake ni 'mji mzuri' au 'beautiful city'.


08/11/2007

BASI LA KIVUKONI

OLYMPIC STADIUM 2012 - LONDON

Uwanja wa Olympic 2012 London ambao umependekezwa kujengwa. Unasemaje?

MTAA WA LIVINGSTONE

Mtaa wa Livingstone, Dar es Salaam, uonekanavyo hivi sasa


09/11/2007

UGONJWA WA MOYO

Joram Edikat ni mtoto wa miaka 10 ambaye anaishi katika wilaya ya Katakwi, Uganda. Yeye ni mtoto wa saba kuzaliwa katika familia yao ya watoto tisa. Joram ana ugonjwa wa moyo ambao mishipa yake damu ni hafifu na mengine imeziba ambayo inamfanya tumbo lake kuvimba. Baba yake amesema, Joram alivyokuwa na miaka miwili aliota mshipa katika sehemu zake za siri na kuvimba, lakini walibahatika kumuwahi na kumfanyia operesheni. Baada ya mwaka 2004 ndiyo maradhi ya moyo yamezidi na kufanya tumbo lake lijae maji. Dokta wa kijiji amesema, kila miezi miwili, Joram huwa anakwenda hospitali kutolewa maji katika tumbo lake na kama watamuwacha basi anaweza kufa. Wamemshauri baba yake ampeleke hospitali kubwa ya maradhi ya moyo Uganda, lakini baba yake amesema kuwa hana uwezo huo.

KATUNI

Cheka na vikatuni


- Tutumie picha na habari tofauti za kutoka popote na tutaziweka kwenye mtandao - Email: zenjydar@gmail.com -

- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk