|
Zenjydar Community Association H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE È 07886 535282
|
|
|
Majumba ya Michenzani yanakaribia kwisha kama yalivyoahidiwa na serikali ya Zanzibar
Teknolojia ya kisasa ya kutumia nishati ya Jua (solar energy) zimeenea Zanzibar vijijini. Hii ni hospitali ya Dunga, Zanzibar
Ujenzi wa barabara ya Kilwa road inaendelea vizuri na mandhari yake inazidi kubadilika kuwa nzuri
Mwenzetu kauliza, mlo huu utakula na kinywaji gani? Chagua wewe halafu mezea mate...
Hapo juu ni mwenyeji wa Lamu akiwa na punda wake mitaani. Lamu, ni kisiwa ambacho kipo Kenya na usafiri wake mkubwa ni punda kwasababu ya ukosefu wa barabara nyingi kubwa.
Mjini Lamu
Watoto pia hufunzwa kuanzia utotoni kumuendesha punda
Richard ambaye ni Mtanzania kapata ushindi wa Big Brother 2 Afrika 2007, ambao ulifanyika South Africa. Mshindi huyo kajipatia dola laki moja na kurudi nazo Tanzania. Richard bado yupo South Africa na anatarajiwa kurudi Tanzania tarehe 14/11/2007.
Watu walikusanyika Coco beach, Dar es salaam, wakiangalia laivu (live) kutangazwa kwa mshindi wa big brother Africa 2007.
Kaka yake Richard (katikati) akipongezwa kwa ushindi wa kaka yake baada ya kutangazwa kuwa kashinda big brother Africa 2007.
Richard akionekana akinyanyua sanduku ambalo ndani yake kuna dola laki moja za ushindi wa big brother Africa 2007
Richard akiwa na dada yake ambaye alikwenda South Africa kumshangilia wakipozi na dola laki moja
Baadhi ya akina dada ambao walikuwa wakiuza magazeti ambayo kichwa chake cha habari kinajieleza chenyewe, walikuwa wakiuza magazeti hayo kwa wingi ili watu wapate kujua kisa kilichotokea kati ya Richard na mkewe. Richard anategemewa kufika Tanzania tarehe 14/11/2007.
Sabah Muchacho ambaye ni nyota wa taarab Tanzania, akionekana akitumbuiza katika ukumbi wa Diamond Jubilee wa Dar es salaam.
Nyota mwingine wa taarab Tanzania ni Mwanahawa Ali ambaye pia alikuwa akitumbuiza usiku huo Diamond Jubilee hall
Nyota mwingine ni Bi Zuhura Shabani pia alikuwa akitumbuiza usiku huo
Mamia ya watu walikusanyika uwanja wa ndege wa Dar es salaam, kumshangilia Richard, mshindi wa big brother 2 Afrika
Walinzi wa mlango wa kutokea abiria wa uwanja wa ndege wa Dar es salaam, wakijaribu kumzuia baba yake Richard kuingia ndani kumpokea mwanawe kwa sababu ya usalama. Baba yake Richard alikasirika na kutaka kuondoka.
Richard akionekana akitokea mlango wa nyuma na walinzi wa usalama na kukimbizwa kwenye gari lilikuja kumpokea
Richard akiwa na mshabiki wake ambaye alikuwa uwanja wa ndege wa South Africa, kumuaga kurudi Tanzania
Mshindi wa big brother 2 Afrika, Richard (ambaye ni Mtanzania) akijitayarisha kukabiliana na waandishi wa habari wa kutoka sehemu tofauti ambao walikutana Holiday Inn ya Dar es salaam, katika kumhoji na mambo aliyokabiliana nayo alipokuwa katika nyumba ya big brother huko South Africa
Jengo jipya ambalo lipo katika kona ya mitaa ya Azikiwe na Jamhuri, Dar es salaam limeshakwisha kujengwa na liko tayari kwa ufunguzi.
Picha zenyewe zinajieleza
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Amani Abeid Karume akibadilishana mawazo baada ya mazungumzo na Spika wa Bunge la West Bengal ambae pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Parliamentary Assiciation- CPA).Mhe Hashim Abdullah Halim, Ikulu ya Zanzibar leo. Picha kwa hisani ya Ramadhan Othman wa Ikulu ya Zanzibar INDIA imesifu uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Zanzibar na kuahidi kuuimarisha zaidi uhusiano huo sambamba na kufurahishwa kwake kutokana na kukomaa kwa Demokrasia na Utawala Bora hapa nchini. Kauli hiyo imetolewa leo na Spika wa Bunge la Bengal ya Magharibi ambae pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Mhe. Hashim Abdallah Halim, alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Amani Abeid Karume Ikulu mjini Zanzibar. Katika mazungumzo yake hayo Mhe. Halim alimueleza Rais Karume kuwa India mefurahishwa na uimara uliopo Zanzibar katika uendelezaji mzima wa demokrasia na Utawala Bora hali ambayo itaimarisha zaidi maendeleo ya ya kiuchumi na kijamii. Akitoa maelezo yake katika suala zima la Utawala Bora, Spika huyo alimpongeza Rais Karume kutokana na mafanikio mazuri yaliopatikana katika kuendeleza vikao vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar sambamba na vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania. Pia, Mhe. Halim alieleza kuwa kuwepo hali nzuri ya mahusiano na mashirikiano kati ya Zanzibar na India imejenga zaidi maendeleo katika sekta ya elimu kutokana na vijana wengi wa Kizanzibari kujipatia elimu nchini humo. Mhe. Halim alisema kuwa mbali ya vijana wengi kujiunga na vyuo viliopo nchini humo pia uendelezaji wa sekta ya biashara baina ya wafanyabiashara wa Zanzibar na India nao umeimarika hali ambayo inasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uchumi. Aidha, Mhe Halim alisema kuwa kuna kila sababu ya kuunga mkono mafanikio ya kiuchumi na kisiasa yaliopatikana hapa nchini. Alieleza kuwa India itaendelea kushirikianiana na Zanzibar katika kuimarisha sekta zake za maendeleo na uchumi kutokana na mafanikio makubwa ambayo tayari yameshapatikana nchini mwake ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa sayansi na teknolojia. Nae Rais Karume alimpongeza Spika huyo kwa ujio wake ambao unaonesha ni kwa jinsi gani Indiia na Zanzibar zimekuwa na ushirikiano na uhusiano wa muda mrefu. Rais Karume alimueleza Mhe. Halim kuwa Zanzibar itaimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano ambao tayari umeshapata mafanikio makubwa katika kuimarisha sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya elimu. Akieleza mafanikio yaliopatikana katika sekta ya elimu, Rais Karume alisema kuwa vijana wengi wa Kizanzibari wamekuwa wakipata elimu katika vyuo mbali mbali nchini humo ikiwemo elimu ya Sheria ambapo kuna haja kwa nchi hiyo kutoa nafasi zaidi ya masomo ya Teknolojia kwa vijana wa Kizanzibari. Pia, Rais Karume alimueleza Mhe. Halim kuwa imefika wakati kwa Wazanzibari kujiimarisha katika elimu ya Teknolojia katika vyuo vikuu vilivyopo hapa nchini, elimu ambayo imeshapiga hatua kubwa nchini India. Aidha, Rais Karume alimueleza Mhe Halim kuwa tayari mafanikio makubwa yameshapatikana katika sekta mbali mbali za maendeleo kutokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na Serikali katika kupamabana na umasikini. Pamoja na hayo, Rais Karume alimpongeza Mhe. Halim pamoja na nchi yake kwa kuendeleza vyema uhusiano uliopo pamoja na kusifu hatua za maendeleo ya sayansi na teknolojia yaliofikiwa nchini humo. Rais Karume alisema kuwa Zanzibar inathamini sana uhusiano na ushirikiano wake na India hali ambayo inapekelea kuendelea kupanua wigo wa maendeleo kutoka nchini humo. Habari na Rajab Mkasaba, Zanzibar.
Cheka na vikatuni - Tutumie picha na habari tofauti za kutoka popote na tutaziweka kwenye mtandao - Email: zenjydar@gmail.com - - Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran! |
|
|
|