Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

17/11/2007

UBUNIFU WA WAJAPANI

Ubunifu wa Wajapani


18/11/2007

UWANJA WA TAIFA

Huu ni uwanja wa taifa wa zamani ambao unatumika kwa mazoezi mbalimbali. Uwanja wa taifa wa zamani umefanyiwa ukarabati na kutiwa nyasi bandia za kimataifa kama uzionapo hapo juu. Kwa mbali ni uwanja wetu wa taifa mpya.

M.V. SEAGULL

Meli ya kasi ya abiria ambayo imeitwa M.V. Seagull, itaanza kazi zake Ijumaa tarehe 23/11/2007 kutoka Dar kwenda Zenjy. Meli hiyo ambayo ina uwezo wa kubeba abiria 410 kwa mara moja, huchukua dakika 90 au (saa moja unusu) kutoka Dar hadi Zenjy. Itaanza huduma zake za kutoka Zenjy mpaka Pemba baada ya Eid el-hajj, 2007. Seagull inamilikiwa na mfanya biashara wa Zanzibar.


19/11/2007

MAMBO YA CENTRAL LONDON

Mambo hapo juu ni Central London, kweli tembea uone mambo!

POZI ZA MWALIMU

Pozi za Mwalimu Nyerere


20/11/2007

KUNDUCHI BEACH

Kunduchi beach hotel ilivyo sasa ambayo imeongezewa maraha mengine ya watoto kujifurahisha

TPN

Kushoto: Mheshimiwa bi Maua Daftari ambaye ni naibu waziri katika wizara ya miundombinu, akiwa na Spika mheshimiwa Samuel Sitta katika ufunguzi wa hafla ya kutunisha mfuko wa TPN (Tanzania Professionals Network), huko Dar es salaam.


21/11/2007

TAIFA STARS

Kocha wa taifa stars Marcio Maximo akiwa na wachezaji wa taifa akiwapa maneno ya kutia nguvu wakiwa katika uwanja wa taifa wa zamani. Maximo atakwenda Durban, South Africa, kuhudhuria uchaguzi wa timu za mabara katika michuano ya kutafuta tiketi ya kushindana kombe la dunia. Vilevile atajaribu kuongea na viongozi wa Brazil ili timu ya Brazil ipige kambi Tanzania wakati wa mechi za kombe la dunia 2010, South Africa. Je, Maximo na watoto wetu wataingia kombe la dunia mwaka 2010, South Africa?

KARAM

Mbona kaka unaturuka? weka hiyo sinia chini... au ndio pozi za picha hizo?


22/11/2007

M.V. SEAGULL

M.v. Seagull imeingia Dar es salaam na iko tayari kuanza kazi zake za kubeba abiria kutoka Dar kwenda Zenjy.

SERENGETI

Serengeti, Tanzania


23/11/2007

GARI GHALI DUNIANI

Hii gari ni gai ambayo imethaminiwa kuwa ni gari ghali duniani. Gari hii aina ya Bugatti ni gari ya Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum wa Dubai, na thamani ya gari hii ni (amini usiamini) 5 billion pounds za UK (paundi bilioni tano za UK). Isitoshe, ni gari ambayo ina 'plate number' ghali uarabuni kote. Kawaida arabuni gari ikiwa na namba moja ni gari ya mtu mkubwa sana serikalini au tajiri kupita kiasi. Angalia vitu hivyo! (Ina radiator 9, speed 450km/hr).

KATUNI

Cheka na vikatuni


- Tutumie picha na habari tofauti za kutoka popote na tutaziweka kwenye mtandao - Email: zenjydar@gmail.com -

- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk