Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

Č 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

24/11/2007

JAKAYA KIKWETE NA FREEMAN

Kikwete akisalimiwa na mwenyekiti wa chama cha Chadema mheshimiwa Freeman Mbowe, huku mzee Mengi wa IPP akisubiri zamu yake katika hafla iliyoandaliwa huko Ikulu kwa heshima ya rais wa Comoro. Kama kawaida ya utamaduni wetu mzuri wa watu wa Tanzania, tunatofautiana kisiasa lakini uutu wetu upo palepale.

MSIMU

Msimu wa matunda nyumbani umeanza

AJALI

Mwenye gari hii alikuwa akilalamika kuwa, kachomekewa na daladala mpaka kaingia mtaroni


25/11/2007

BONGO POA

Wazungu wanakubali kuwa "bongo poa"

UKONGORONI

Rais wa Zanzibar mheshimiwa Aman Abeid Karume akiwa na waalikwa wake wa kutoka Ukongoroni, Zanzibar ambao walialikwa rasmi huko Ikulu Zanzibar.

NICK

Nick ni kijana mwenye miaka 23 ambaye alizaliwa bila ya mikono wala miguu. Katika familia yao Nick ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika watoto watatu ambao wawili ni mdogo wake wa kiume na mwingine mdogo wake wa kike ambao wamezaliwa bila ya ulemavu. Nick anaamini kupata ulemavu huo ni kazi ya Mungu na anasema atajitahidi kadri anavyoweza kuongea na vijana juu ya mambo ambayo vijana wa leo yanawakabili.


26/11/2007

KINGWENDU NA MZEE SMALL

Kingwendu na Mzee Small ni wachekeshaji ambao wenye vipaji vya kuigiza na wanajulikana kwa kazi zao nyingi ambazo wamezifanya kwenye filamu tofauti Tanzania. Kipaji chao kwenye mambo ya uchekeshaji inakadiriwa ni cha hali ya juu kulko vipaji vya waigizaji wa kipindi cha Ze Comedy. Kwa kuwa walisahaulika kwa kipindi fulani, Inasemekana kuwa watapewa nafasi ya kurudi tena jukwaani na kuonekana kwenye EATV 'channel 5' kama Ze Comedy.

KIBANDA PEKEE

Kibanda kilichobaki pekee mjini Dar es salaam, kimefikia siku zake kubomolewa baada ya watu wengi waliokuwa wakijiuliza iweje vibanda vingine vyote vivunjwe na kibanda hicho kibaki pekee. Lakini sauti za watu zimesikika na kama ionekanavyo kwenye picha siku zake zimefika.


27/11/2007

WORLD CUP 2010

Grupu ambalo Tanzania imepangiwa nao katika kuwania tiketi ya kwenda kucheza World Cup 2010, South Africa. Kazi ipo!

KARIAKOO

Pirika za Kariakoo kwa gari

Pirika za Kariakoo kwa miguu


28/11/2007

MAENDELEO YA ELIMU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Amani Abeid Karume,akibadilishana mawazo jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Celtel, Bashar Arafish, baada ya kukabidhiwa Kompyuta 65, ambazo zitatumika kwa Skuli za Sekondari za Zanzibar ,hafla ya makabidhiano ilifanyika Ikulu Mjini Unguja.

Kampuni ya simu ya CELTEL imeeleza lengo lake la kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu na kukabidhi kompyuta 65 kwa ajili ya skuli za Sekondari za hapa nchini.

Akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Amani Abeid Karume, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CELTEL Bwana Bashar Arafeh huko Ikulu mjini Zanzibar alieleza kuwa kampuni yake itakuza ushirikiano na Zanzibar katika kuendeleza sekta ya elimu. Alieleza kuwa kampuni ya CELTEL imefarajika kwa kiasi kikubwa kutokana na maendeleo ya sekta ya elimu jinsi yalivyofikiwa hapa nchini na iko tayari kuendelea kuyaunga mkono maendeleo hayo.

Bwana Arafeh ambaye alifika Ikulu pamoja na Ujumbe wa Kampuni hiyo, alisema kuwa Kampuni yake imeweka kipaumbele zaidi kusaidia katika sekta ya elimu kutokana na kuelewa kuwa elimu ni kitu muhimu katika maendeleo ya mwanaadamu. “CELTEL inaunga mkono hatua zilizofikiwa katika sekta ya elimu hapa Zanzibar na ndio maana imeshajiika kuendelea kutoa misaada yake kwa ajili ya kuimarisha sekta ya elimu” alisema Bwana Arafeh.

Arafeh alimueleza Rais Karume kuwa Kampuni ya CELTEL ina mpango wa kuanzisha kituo cha teknolojia ya kompyuta hapa Zanzibar.Alisema kuwa kompyuta hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza masomo kwa wanafunzi wa skuli za sekondari za ari za hapa nchini. Arafeh alisema kuwa Kampuni yake ina mahusiano mazuri na makampuni mengine ya simu hapa nchini ikiwemo Kampuni ya ZANTEL ambayo tayari wana mpango wa kushirikiana katika kutoa huduma za mawasilinao.

Alisema kuwa kampuni ya CELTEL tayari imeshatandaza huduma zake katika nchi zipatazo 22 duniani zikiwemo nchi za Mashariki ya Kati na nchi za Afrika na kueleza kuwa hatua hiyo imeweza kupanua kwa kiasi kikubwa soko lake la biashara. Nae Rais Karume kwa upande wake aliipongeza Kampuni ya CELTEL kwa uamuzi wake bora wa kusaidia kompyuta kwa skuli za sekondari Zanzibar sambamba na kuendeleza ushirikiano wake na Serikali.

Rais Karume alisema kuwa Kompyuta hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza elimu ya teknolojia kwa wanafunzi wa sekondari wa hapa nchini pamoja na kusaidia kwa programu mbali mbali za elimu. Alisema kuwa kompyuta hizo zitasaidia katika kufikia malengo yaliowekwa na Serikali ya kuimarisha sekta ya elimu hapa nchini na kuisifu kapuni hiyo kwa kuunga mkono hatua za maendeleo zinazochuliwa na serikali.

Rais Karume alisema kuwa tayari Serikali ya Mapinduzi imeshapiga hatua kubwa katika sekta ya elimu kwa upande wa elimu ya msingi kwa kuhakikisha watototo wote wanaoandikishwa skuli wanapata nafasi za kusoma na mikakati mikubwa imewekwa hivi sasa katika kuinua elimu ya sekondari.

Alisema kuwa miongoni mwa mikakati ya kuinua elimu ya sekondari ni uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujenga skuli za kisasa za sekondari kwa kila Wilaya hapa Zanzibar. Aidha, Rais Karume aliipongeza Kampuni hiyo kwa kupanua zaidi huduma zake za mawasilinao hapa Zanzibar pamoja na sehemu nyengine duniani sambamba na mipango yake ya kushirikiana na makampuni mengine ya simu kwa ajili ya kupanua soko la kibiashara. Kwa mujibu wa maelezo ya Kampuni hiyo Kompyuta hizo 65 zimegharimu dola elfu 50 za Marekani.
 

Habari kwa hisani ya Rajab Mkasaba -Zanzibar

MBIO ZA UFUKONI...

Siamini wale wanaosema watu wabongo peke yao ndio wenye akili zinazokwenda rivasi. Naangalia picha hii, sipati jibu huyu jamaa kapandaje juu ya gari ya mwenziwe!? Ajali hiyo imetokea Dubai, U.A.E. barabara ya Sheikh Zayed Road ambayo inatokea Abu Dhabi, U.A.E. Waswahili wamesema


29/11/2007

MASHINDANO YA TAARAB

Kiongozi wa East African melody Bw. Haji akihojiwa na mwandishi wa redio ya Mlimani ndani ya ukumbi wa idara ya habari kuhusiana na mapambano yao yatakayofanyika tarehe 30/11/2007 ndani ya ukumbi wa daiamond jubilee.

Baadhi ya viongozi wa vikundi vya taarab vitakavyopambana katika ukumbi wa diamond jubilee wakizungumza na waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa idara ya habari kuhusiana na mpambano huo wa aina yake. Viongozi waliokuepo katika kukutana na waandishi wa habari ni mshauri mkuu wa bendi ya Jahazi Modern Taarab Juma Mbizo, Mkurugenzi wa kampuni ya Liro promotions Suleiman Ling'ande, Meneja mkuu wa kampuni ya QSSP Bahati Said, Kiongozi wa bendi ya East African melody pamoja na Abubakari Mgeni ambaye ni kongozi wa kundi la Dar modern taarab.

Mshindi wa mpambano huo ataibuka na kitita cha milioni moja na mshindi wa pili atajinyakulia kiasi cha shilingi laki tano na wa tatu atapata laki mbili na nusu,


30/11/2007

MNAZI MMOJA - DAR ES SALAAM

Mnazi mmoja hivi sasa, Dar es salaam

MISS WORLD

Richa Adhia ataiwakilisha Tanzania kama Miss Tanzania 2007 kwenye kutafutwa Miss world 2007 huko China usiku wa kesho tarehe 01/12/2007.

KATUNI

Cheka na vikatuni

HII SIO KATUNI

Subira...


- Tutumie picha na habari tofauti za kutoka popote na tutaziweka kwenye mtandao - Email: zenjydar@gmail.com -

- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk