|
Zenjydar Community Association H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE È 07886 535282
|
|
Salam za Eid kutoka London
Salam za Eid kutoka Dar Es Salaam
Salaam za Eid kutoka Bangladesh
Salam za Eid kutoka Korea
Salam za Eid kutoka kwa Bi Kidude
Salaam za Eid kutoka Turkey (tarehe ya picha imekosewa kurekebishwa)
Watu wa kutoka kila kona ya jiji; wenye hali na mali tofauti; hujifurahisha pamoja
Watoto wakijifurahisha kwa kuogelea
Wengine wakiangalia ustaarabu
Baadhi ya watu hufika Coco Beach kwa usafiri wa daladala
Au, usafiri wa binafsi
Wengine hutumia bongo!
Njia ya kuelekea Coco Beach
Wengine wakijimwaga pembezoni
Na Issa Michuzi alikuwa kileleni - Eid Mubarak!
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania bado anakumbukwa. Mwalimu alifariki katika hospitali ya London, tarehe 14/10/1999 na akazikwa kijiji cha Butiama ambacho kipo mkoa wa Mara, tarehe 23/10/1999. Mwalimu Nyerere alizaliwa mwaka 1922 wakati Tanganyika inatawaliwa na British. Baba yake alikuwa ni chifu wa kabila la Zanaki. Mwalimu alijipatia (degree) ya historia na uchumi hapa England na aliporudi Tanganyika aliamua kuwa mwalimu. Mwaka 1953 aliamua kusaidia, kuanzishwa kuundwa kwa chama cha TANU (Tanganyika African National Union), ambacho chanzo chake ndicho kilichosaidia Tanganyika kupata uhuru. Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961, mwalimu alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika. Baada ya miaka mitatu (mwaka 1964) mwalimu aliamua kuungana na Zanzibar na kuwa nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwalimu Nyerere kuwa rais wa kwanza wa Tanzania. Mwalimu Nyerere alifaulu awamu tatu kuwa rais wa Tanzania mpaka kujiuzulu kwake mwaka 1985 na kumuachia madaraka rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi. Moja ya sifa kubwa za mwalimu Nyerere ni kuifanya Tanzania iwe ni nchi ya amani na nchi ya watu wote kuwa sawa na kuishi pamoja bila ya kujali rangi zao wala ukabila. Alikuwa ni mtu ambaye mtazamo na maoni yake yaliheshimiwa na wa kubwa wa nchi tofauti duniani na hata wengine walikuwa wakimuomba ushauri kutoka kwake. Alikuwa vilevile ni mmoja wa waanzilishi wa OAU mwaka 1963. Sio tu Nyerere atakumbukwa kuzisaidia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru au kuifanya nchi yake iwe ya amani na watu tofauti kuishi pamoja, pia atakumbukwa kuwa ni mmoja wa viongozi bora wa bara la Afrika ambaye aliheshimika Afrika, nchi za magharibi na duniani kote. Nyerere alifariki mwezi huu wa Oktoba mwaka 1999, na kama watanzania, tunajisifu kwa kiongozi wetu na kusema kuwa, Mwalimu tunamkumbuka katika mwezi huu wa BLACK HISTORY MONTH.
Mwalimu akiongozana na mawakili wake wakielekea mahakama ya kivukoni ambako alipanda kizimbani baada ya kushtakiwa kwa kosa la kutaka kusababisha vurugu baada ya kuandika kile kilichoonekana maneno ya uchokozi kwenye gazeti la TANU ambapo alimsema DC (District Commissioner) mmoja ambaye alikasirika na kumshtaki. Mwalimu alipatikana na hatia ya kuandika uchochezi na kutozwa faini ambayo ililipwa na wanachama wa TANU
Mwalimu akiwa na mgeni wake Aga Khan na katibu mkuu wake Rashid Kawawa
Mwalimu akimpokea Mheshimiwa Abeid Aman Karume katika kiwanja cha ndege cha Dar Es Salaam
Mwalimu na mheshimiwa Nelson Mandela
Gari ya aina ya Austin Morris aliyokuwa akitumia mwalimu kabla ya uhuru. Dereva wake alikuwa Mzee Saidi Tanu, ambaye pia ni marehemu.
Gari nyingine iliyokuwa ikitumiwa na TANU kabla ya uhuru
Gari aina ya Rolls Royce, ambayo aliyokuwa akiitumia kupokelea wageni wake wafikapo Dar Es Salaam
Gari ya aina ya Mercedes Benz, ambayo mwalimu alikuwa akiitumia baada ya kustaafu kuwa rais wa Tanzania
Hifadhi
Nyumba ya mwalimu aliyokuwa akikaa baada ya kustaafu
Moja ya njia ya kuingilia na kutokea ndani
'View' ya nje kwenye roshani
Kibanda cha nje ambacho mwalimu alikuwa akikitumia kuchezea mchezo wa bao na vilevile ni sehemu aliyokuwa akiitumia kukaribishia wageni wake tofauti kwa maongezi wakiwamo maraisi, wafalme na wakuu mbalimbali.
Sanamu ya mwalimu ambayo ipo kijiji cha Mwintongo, Butiama, ambapo ndipo alipozaliwa
Jengo ambalo ndani yake kuna kaburi la mwalimu
Baadhi ya vitu ambavyo ni milki ya mwalimu ambavyo vimewekwa kama makumbusho
Katika kuadhimisha siku ya Nyerere Day, jeshi la ulinzi limeandaa maonyesho maalum ya amiri jeshi mkuu wa kwanza kwenye jumba la JWTZ.
Baadhi ya vijana waliohudhuria maonyesho hayo wakisimuliwa historia ya vita vya Kagera
Mwili wa mwalimu uliposhuka Dar Es Salaam kutoka London
17th February 1885 - 1st January 1891 German East Africa Company
1st January 1891 - 9th October 1916
1913 (Proposed colonial flag)
9th October 1916 - 1919
1919 - 1st May 1961
1st May 1961 - 30th June 1964
30th June 1964 - to date
Maeneo ya Posta ilivyo sasa
Maendeleo ya jiji la Dar Es Salaam yakishamiri kwa vitu kama hivi; supermarket za kileo
Moja ya kampuni kubwa ya magari duniani, TOYOTA, wamezindua gari mpya ya HI-CT ambayo inakwenda kwa kutumia nusu petroli na nusu betri. Gari hiyo ina soketi ya AC100V ambayo inatumiwa kuchajia umeme wake.
Nafikiri ile taimu ya wenye mikokoteni kuwa na leseni imefika!
Safari ya maili mia huanza na hatua moja
......!
Hii ndio ndege ya A380 (Airbus 380) ambayo ilikuwa ikingojewa kwa muda mrefu na wateja wa Singapore Airline. A380 ambayo inajulikana kama 'double decker' (kwasababu inachukuwa abiria juu na chini) ni ndege ambayo imeleta mapinduzi ya ndege zote ambazo zinatumika hivi sasa ambayo hata mashirika makubwa ya ndege kama Emirates Airline na Qantas ya Australia wameamua kuweka oda zao za ndege hizo mpya. Kama unavyoiona kwa nje inaonekana kama ndege yoyote ya kawaida, lakini ndani ndio vimbwanga vyote vinaanza kubadilika kwa starehe na vifaa vilivyokuamo humo ndani. Starehe na vifaa vilivyomo humo ndani, hutojali kama unakwenda Unguja kutoka Dar es Salaam kupitia transit New York.
Ukitaka kujifurahisha
Ukitaka kufanya kazi zako
Ukitaka kucheza
Ukitaka kulala
Na mlango wako funga jisikie peke yako au na mwenzako
Ukitaka mtandao (internet)
Au kijiusingizi kidogo
Asubuhi ya leo huko posta mpya, huyu kijana alijaribu kukwapua simu ya mkononi na kujaribu kukimbia; wazalendo wenye hasira walimfukuza na kumkamata na kupigwa kipigo cha kisawasawa na kuachwa baada ya Polisi kufika. Hali yake haijulikani.
Cheka na vikatuni - Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran! |
|
|