|
Zenjydar Community Association H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE È 07886 535282
|
|
|
kikundi maalum cha taarab (Culture Musical Club) kimeelekea kwenda Zurich, Switzerland, kwa ajili ya maonyesho maalum. Culture ni moja ya makundi yanayoipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kufanya maonyesho mbalimbali katika nchi tofauti. Msafara huo utakuwa na wasanii kumi na mbili na watatu kati yao ni wanawake ambao wataongozwa na muimbaji maarufu wa taarab Bi Rukia Ramadhan.
Naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa akiwa katika ziara ya kikazi mjini London, alipata nafasi ya kumzuru Mheshimiwa Rashid Mfaume Kawawa (aliyekuwa katibu mkuu wa Tanzania). Pichani juu kutoka kulia ni katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Mh. Rashid Kawawa, mkewe Kawawa na balozi wa Tanzania nchini U.K., Mheshimiwa Mwanaidi Maajar. Picha ya chini wakiwa na msaidizi maalum wa mzee Kawawa.
Muimbaji maarufu wa Afrika ya kusini ameuwawa kwa kupigwa risasi na majambazi waliotaka kumpora gari yake kwenye mida ya saa mbili za usiku huko mji wa Rosettenville, Johannesburg.
Gari ya Lucky Dube
Polisi wakifanya uchunguzi wao huku wakikagua gari hiyo na tukio kamili
Rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mama wa kwanza Bi Salma Kikwete wakiwa na Papa Benedict wa 16 huko Vatican, Italy, katika ziara yake ya kikazi. Papa Benedict pia anategemewa kuzuru Tanzania hivi karibuni.
JK alimpelekea zawadi maalum Papa Benedict wa 16 katika ziara yake ya kikazi huko Vatican, Italy.
(No nonsense) Kwenye tamasha la michezo ya vyuo huko Dar es Salaam, hawa jamaa wawili walikuwa wakifurahisha watazamaji baada ya fainali ya michezo hiyo kwisha.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam katika miaka ya sabini
Watanzania walioshiriki maonyesho ya sanaa ya watu wa kutoka mataifa mbalimbali yaliyofanyika mjini London
Mheshimiwa Jakaya Kikwete akipiga ngoma ya ufunguzi wa maonyesho ya sanaa katika chuo cha sanaa mjini Bagamoyo. Tamasha hilo litafunguliwa na makamu wa rais wa Tanzania, Dk. Ali Mohammed Shein.
Balozi wa
Marekani kujibu maswali moja kwa moja kupitia
mtandao:
Balozi wa Marekani Bwana Mark Green kujibu maswali kutoka kwa Watanzania kupitia mjadala wa moja kwa moja kwa njia ya mtandao ambao umepangwa kufanyika Jumatatu, Oktoba 29, 2007 kuanzia saa tisa mchana za Tanzania.
Katika kipindi hicho
cha majibu na maswali, Balozi Green atajadili kuhusu
msaada wa dola milioni 698 utakaosaidia kupunguza
umaskini nchini Tanzania, ambao uliidhinishwa hivi
karibuni.
Balozi Green amesema kuwa, huenda maneno “MCC” na “sheria ya Millennium Challenge” yatawachanganya baadhi ya watu hapo mwanzoni, lakini baada ya muda kidogo, Watanzania watajifunza jinsi mpango huo unavyoweza kuleta tofauti kubwa katika maisha yao. “Pindi mkataba mpya wa MCC utakapotiwa saini na Serikali ya Tanzania, utajenga ushirikiano wa karibu zaidi kati ya mataifa yetu mawili.” Mpango huo wa MCC uliotolewa na wananchi wa Marekani, ni mpango wa miaka mitano ambao lengo lake ni kupunguza umaskini, kuchochea kukua kwa uchumi, na kuongeza kipato cha wananchi kupitia uwekezaji maalum katika miundombinu ya sekta za usafiri, nishati na maji nchini kote Tanzania. Ili uweze kujiandikisha kushiriki kwenye mjadala huu wa mtandao, tumia anuani yako ya barua pepe kuingia kwenye ukurasa wa mtandao wa http://webchat.state.gov.
Unaweza pia kuingia
kwenye mjadala huo wa mtandao kupitia ukurasa wa
mtandao wa Tanzania
http://tanzania.usembassy.gov.
Mtoto mwenye umri wa miezi 11 na mwenye uzito wa kilo 52.2, ambaye yupo katika kitongoji cha Rajasthan, India, anashikilia rekodi ya dunia ya kuwa mtoto mzito kuliko wote wenye umri huo duniani.
Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto, Mh. Salome Joseph Mbatia (55) amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari kwenye mashamba ya chai kwenye maeneo ya Kibena kabla ya kufika Njombe. Mwili wa Mheshimiwa Salome utapokewa mjini Dar es Salaam kutoka Iringa, tarehe 25/10/2007 na kutayarishwa kwa maziko. Mumewe Dk. Joseph Mbatia amenukuliwa akisema kuwa hayati Salome amefariki tarehe ile ile aliyofariki mama yake mzazi.
Mheshimiwa Jakaya Kikwete na waheshimiwa wengine wakisubiri kupokea mwili wa hayati Salome Mbatia
Mwili wa hayati Mbatia ukishuka uwanja wa ndege wa Dar es Salaam
Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwapa pole watoto wa hayati Salome
Mheshimiwa Jakaya Kikwete akionekana akijivuta kwenye kiti chake kukaa vizuri katika kukutana na wakubwa wengine kwenye mkusanyiko wa kumuaga hayati Salome Mbatia. Mwili wa hayati Salome utasafirishwa hivi leo tarehe 26/10/2007 na kupelekwa kwao huko Moshi katika mkoa wa Kilimanjaro ambapo anatarajiwa kuzikwa (kesho tarehe 27/10/2007). Kutoka kushoto Mh. Benjamin Mkapa, Al Hajj Ali Hassan Mwinyi, Mh. Amani Karume, Mh. Jakaya Kikwete, Dk. Joseph Mbatia na Dk. Ali Shein.
Mama Maria Nyerere akitoa heshima za mwisho kwa ndugu na jamaa wa hayati Salome Mbatia
Al Hajj Ali Hassan Mwinyi na mkewe Bi Siti, wakitoa heshima za mwisho za kumuaga hayati Salome Mbatia
Kama umefika Zanzibar na hujafika Forodhani basi hujamaliza ziara yako, rudi tena. Hapo ndio Forodhani, pweza mkia mmoja ni 2,500/=, Ngisi mkubwa 3,500/= na mdogo 2,500/=. Juice ya miwa jagi la moto ni shilingi 350/= na jagi la baridi (unatiliwa barafu) shilingi 300/=. Piga mahesabu akili kichwani mwako.
Never give up! - Tutumie picha na habari tofauti za kutoka popote na tutaziweka kwenye mtandao - Email: zenjydar@gmail.com - - Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran! |
|
|
|