|
Zenjydar Community Association H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE È 07886 535282
|
|
|
Ujenzi wa daraja jipya la Ruvu umeanza
Ndani ya viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, kampeni ya kupiga vita ukimwi inaendelea. Yeyote mpita njia anaweza kwenda humo ndani na akapima na kupata majibu hapo hapo. Kampeni hiyo ilizinduliwa na rais wa Tanzania, mheshimiwa J. Kikwete na kuiita "Tanzania bila ya ukimwi inawezekana".
Ugomvi wa Joti na Guruguja katika mchezo wa Ze Comedy, Tanzania
Huyu ndie Kingwendu ambaye wengi wenu mnamjua katika michezo yake ya kuchekesha, ni mchekeshaji mwenye kipaji ambacho akitokea kabla hajakuchekesha, utacheka.
Matokeo: Liverpoo 1-1 Arsenal
Jengo ambalo litakalokuwa makao makuu mapya ya jeshi la magereza ambalo lipo mtaa wa Shaaban Robert/Sokoine Drive mjini Dar es Salaam
Kaka Issa Michuzi katuletea picha mpya za ndege kubwa ya kwanza yenye kuchukua abiria juu na chini na yenye raha zote za kila aina ambazo utazihitaji. Urefu wa A380 kwenda juu ukichukulia na upanga wake ni sawasawa na ghorofa sita. Hii ni picha yake kwa nje.
Matairi
Ndani
Ndani
Ndani
Ndani
Ndani
Kaka Issa Michuzi akionekana yupo ndani ya pipa
Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, Mh. Bernard Kamilius Membe, anamkabidhi Miss Tanzania 2007 Richa Adhia, bendera ya taifa katika hafla ya kumuaga kwenda kushindana mashindano ya Miss World 2007. Mashindano ya Miss World 2007 yatafanyika China katika mji wa Sanya, tarehe 1/12/2007.
Familia iliyopo hapa Uingereza wamebahatika kupata watoto wawili mapacha kurwa na dotto ambao kwa uwezo wake mola, mtoto mmoja katoka mzungu na mmoja katoka mmatumbi pyua. Wataalam wanasema hii hutokea kwa nadra sana; mara moja katika milioni moja.
Shoppers Plaza ni moja ya supermarket kubwa zilizopo Dar es Salaam. Ipo barabara ya Old Bagamoyo road ukielekea Mikocheni.
Klabu maarufu ya Bilicanas ikionekana ikiwa katika ukarabati wa muda mrefu wa kuitanua na kuitengeneza klabu hiyo iwe ya kileo zaidi mjini Dar es Salaam.
Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Tanzania, imewafungia wachezaji wake kwa muda wa miezi sita na baadhi yao kufungiwa kwa miezi mitatu kwasababu ya utovu wa nidhamu. Wachezaji hao ambao walitoroka kambini baada ya mechi yao na Simba. Waliofungiwa kwa miezi sita ni Ivo Mapunda na Shadrack; na waliofungiwa miezi mitatu ni Ben Mwalala na Edwin Mukenya.
Shadrack Nsajigwa
Edwin Mukenya
Ben Mwalala
Baada ya takriban mwaka mmoja, treni ya abiria ya kwenda mikoani ilisimama kwasabuabu fulani fulani. Leo imeanza huduma zake tena rasmi kuelekea Mwanza na Kigoma kutoka Dar es Salaam na jamaa na ndugu wa abiria wakionekana pichani wakiaga jamaa zao wanaoelekea mikoani.
Baadhi ya wakubwa wa shirika la treni walikusanyika kuiaga treni hiyo ikiwa ikiondoka kwa kuanza huduma zake kuelekea mikoani.
Abiria wakionekana wakiaga ndugu na jamaa zao
Jengo jipya ambalo litakuwa makao makuu mapya ya wizara ya Maliasili na Utalii liliopo barabara ya Nyerere (zamani pugu road) linakaribia kuisha.
Cheka na vikatuni - Tutumie picha na habari tofauti za kutoka popote na tutaziweka kwenye mtandao - Email: zenjydar@gmail.com - - Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran! |
|
|
|