Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

TAREHE 01/09/2007

HESHIMA KWA NYOTAZ WA ENZI ZAO

Enzi zao! Peter Tino akionekana pichani akitia saini mpira maalum ambao wachezaji wote wa zamani wa taifa stars walitia saini katika mpira huo ambao ulitolewa maalum na kampuni ya vifaa vya michezo vya AB sports. Kampeni ya mkutano huo uliofanyika Sea Cliff, ni moja ya kuwapa moyo wachezaji wapya wa taifa stars ili wafanye vizuri katika mashindano yao. Peter Tino alikuwa ni mshambuliaji hatari wa timu ya Pan Africa na vilevile alichezea taifa stars. Tino yupo kwenye vitabu vya historia baada ya kuifikisha bongo kwenye fainali za Afrika huko Lagos, Nigeria, mwaka 1981 kwa goli lake pekee alilowafunga Zambia. Kwa mbali nyuma, mwenye nyekundu, ni Ahmed Amasha ambaye alikuwa beki tatu hatari wa timu ya Yanga na taifa stars (aaaahh!! enzi hizo!) na baadaye alihamia Muscat, Oman kuchezea timu ya Fanja.

Peter Tino na Kitwana Manara

Peter Tino akisalimiana na makocha wa taifa stars. Kulia ni kocha wa vijana Tinocco, akifuatiwa na kocha wa viungo Ittamar na Kitwana Manara akishuhudia.

Kulia chini ni Sekilojo Chambua, Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madenga na Makumbi Juma "homa ya jiji". Waliosimama ni Romario, Mohamed Hussein, Kombo na Abubakar Salum "sure boy".

Kushoto ni Juma Pondamali Mensah ambaye alikuwa Tanzania One wa enzi hizo. Kushoto ni Tanzania One wa sasa Ivo Mapunda

Mohamed Hussein "Mmachinga" akiwa na vijana wa taifa stars

Makocha wa taifa stars wakiwa na wachezaji wa zamani wa taifa stars. Kushoto waliosimama ni Othman Juma Chama, Sunday Manara, Mwankemwa (Daktari wa timu), Richard Adolf, Mtemi Ramadhan, Maximo, Mohamed Mkweche, Isihaka Hassan "Chuku", Ahmed Amasha, Ittamar, James Kisaka, Tinocco, Kitwana Manara na aliyekaa chini ni Juma Pondamali.

Kushoto ni mbunge wa Kinondoni mheshimiwa Iddi Azzan akiwa na bosi wa kampuni ya Easy Finance mheshimiwa Isaac Kasanga na mgunge wa Mafia na Abubakar Salum "sure boy".

__________

MASHINDANO YA SHARUBU

__________

__________

_________

Mashindano ya dunia ya kutafuta mshindi wa usanii wa masharubu na ndevu ya mwaka 2007 yalifanyika mjini Brighton, Sussex, England. Washindanaji walitoka nchi tofauti zikiwamo Hungary, Romania, Zurich, Marekani, Greece, Italy, n.k.

_________

MENO YA CHUMA

__________

__________

Rathakrishnan Velu, ni mtu wa Malaysia ambaye anajulikana kwa jina lingine kama "King Tooth" alivunja rekodi ya dunia baada ya kuvuta treni ambayo ina mabehewa saba kwa kutumia meno yake ya kuzaliwa nayo na kamba ya waya za chuma.

__________

TAIFA STARS YAPAMBANA NA UGANDA CRANES

Tiketi ya kuingilia uwanja mpya wa taifa katika mechi ya kirafiki baina ya taifa stars na Uganda cranes

Mlangoni, skauti wakisaidia kuwaruhusu watu kuingia kwenye mechi

Fanya fujo uone! Jeshi la kujenga taifa walipewa kazi ya kuangalia usalama katika wanja jipya la taifa

Kwa utaratibu kabisa

Na kwa mpango kabisa

Washabiki

Washabiki

Washabiki

Washabiki

Washabiki

Washabiki

Washabiki

Parking

Walete walete!

Taifa Stars

Uganda Cranes

Waamuzi: kushoto ni kamisaa wa mechi Maulid Dilunga na katikati ni mwanamke wa kwanza wa kibongo kupata beji ya FIFA.

Mheshimiwa JK akimwaga vitu laivu kwenye waidi skrini. Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ndiye Rais wa kwanza kutilia mkazo na kujihusisha sana kwenye mambo ya kuendeleza michezo nchini Tanzania.

Vyombo vya habari

Wasikwambie hujafika

Abesi-abesi. Katika mechi hiyo, Taifa stars walishinda bao 1-0 katika dakika ya 20 ya kipindi cha pili.

__________

MISS TANZANIA 2007

Richa Adhia, ndiye Miss Tanzania 2007 baada ya kuchuana na washindani wengine huko Dar es Salaam katika hoteli ya Beach Comber katika usiku wa tarehe 01/09/2007.

Katuni ya kwenye gazeti la bongo

Kumi bora

Tano bora

katikati balozi wa Palestina akimpa zawadi Richa Adhia ambaye ni Miss Tanzania 2007. Kulia kabisa ni Miss World 2001 Agbani Derago, ambaye alikuwa ni jaji mkuu katika mashindano hayo.


02/09/2007

WABONGO WA HOUSTON NA ATLANTA - MAREKANI

Timu ya wa Tanzania waliopo Atlanta, Marekani

Timu ya wa Tanzania waliopo Houston, Marekani.

Timu ya Houston waliifunga timu ya Atlanta mabao 5-3 katika mechi za kirafiki


03/09/2007

KIMOMBO

Boda kwa boda; Bongo, hakuna kisichowezekana

__________

Boda kwa boda, vitu Laivu tuuuu!!!

_________

__________

__________

Basi maarufu la U.K. "National Express" linaonekana likilala kiubavu baada ya kuachia njia kuu ya "motorway" (M1). Basi hilo ambalo lilikuwa limebeba abiria karibu 30, lilikuwa linatoka Birmingham na kuelekea Luton mpaka Stansted Airport, baada ya ajali hiyo kutokea dereva aliwekwa chini ya ulinzi baada ya kushukiwa kuwa alikuwa amelewa na huku akiwa akiendesha basi la abiria. Baadhi ya abiria ambao wamepona, mmoja wao alisema aliliona basi likiwa likiyumbayumba mara mbili tatu na aliamua kufunga mkanda wake ambao anadai ndio ulimsaidia kuepuka na kupata majeraha.


04/09/2007

MAENDELEO YA AFYA ZANZIBAR

Waziri wa afya na huduma za jamii wa Marekani akiongozwa na maofisa wa Zanzibar katika kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo visiwani Zanzibar.

__________

Basi la taifa stars limeshanolewa na linangoja kuchukuwa wachezaji kupambana na Msubiji siku ya Jumamosi tarehe 08/09/2007 huko Dar es Salaam.


05/09/2007

BODA KWA BODA

Boda kwa boda

__________

Boda kwa boda

__________

Boda kwa boda, Morogoro

__________

Boda kwa boda, Mbeya.

__________

SPIDER MAN - NDANI YA URUSI

__________

__________

__________

__________

Alain Robert, ambaye anajulikana kwa jina la "Spiderman" alionyesha umahiri wake kupanda jumba jipya la (Federal Tower) lililopo Moscow, Urusi, ambalo lina urefu wa futi 720. Alain (45) hutumia mapendekezo yake hayo bila ya kutumia vifaa vyovyote vya usalama vya kumzuia ili asianguke ikiwa atateleza akiwa juu, vilevile hufanya hivyo bila ya kuomba ruhusa ya vyombo vya sheria na hufanya kujifurahisha yeye mwenyewe tu! Alain ambaye ni Mfaransa, alianza "hobby" yake hiyo tangu akiwa na miaka 12 wakati aliposahau funguo za nyumbani kwao ndani ya nyumba yao na alipanda jumba walilokuwa wakikaa ghoroga ya nane kuzifuatia funguo hizo, na tangu siku hiyo ndio ikawa kama mchezo. Alain ameshawahi kupanda Eiffel Tower iliyopo France na Opera House iliyopo Sydney, Australia.


06/09/2007

TEMBO WA USANII WA MAJITI NDANI YA LONDON

__________

__________

__________

__________

Tembo ambao walitengenezwa kwa majiti walionekana wakiwa katika bustani maarufu ya Hyde Park, London


07/09/2007

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA UPINZANI

__________

__________

__________

Viongozi wa kutoka vyama tofauti nchini Tanzania walifanya mkutano wa hadhara mjini Mbeya. Mkutano huo ulikuwa ni mkutano wa shirikisho la vyama vya upinzani vikiwemo TLP, CHADEMA, CUF na NCCR.

__________

TAARIFA YA RAIS WA TANZANIA MHESHIMIWA KIKWETE YA TAREHE 14/08/2007

JUU YA CCM NA CUF

Taarifa ya Rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ambayo aliitoa siku ya tarehe 14/08/2007, Ikulu, Dar es Salaam juu ya maelewano ya vyama viwili hivyo (CCM na CUF). JK alisisitiza kuwa yeye ni mwenye shauku kubwa ya kuleta mapatano na maendeleo ya kuafikiana baina ya vyama hivi na alikisisitiza chama cha (CUF) na uongozi wa chama hicho akiwemo Profesa Ibrahim Lipumba kuwa kujitoa katika maongezi hayo hakutoleta maendeleo ya maelewano. JK alieleza kuwa ataendelea kuleta maendeleo ya maelewano kati ya vyama hivyo na alikumbusha chimbuko la mazungumzo hayo ni ya ahadi aliyoitoa kwa Watanzania katika bunge tarehe 30 Disemba 2005. Alisema katika taarifa yake, anaamini kwa dhati ya moyo wake kuwa hakuna tofauti zozote za kisiasa na kijamii katika nchi yetu zisizomalizwa kwa mazungumzo na anaamini mpasuko huo wa kisiasa unaweza ukawafikiana ikiwa vyama hivyo vitakaa pamoja na kuzungumzia tofauti zao. JK alisema katika taarifa hiyo, mpaka sasa wameshakaa vikao vingi vya maelewano na wameshaelewana katika sehemu tofauti za mazungumzo yao na anaamini kuna sehemu chache tu zilizobakia ambazo pia zinaweza kumalizwa kimazungumzo.

Rais Kikwete alisema, mpasuko huo wa kisiasa unaweza ukatatuliwa kimazungumzo ya maelewano ya pande zote mbili; na kama mpasuko huo ukiendelea bila ya mazungumzo, tutarudi kule tulikokuwa, yaani kwenye uhasama, shutuma zisizoisha, kubaguana, kutozikana na hata kutosalimiana. Itakuwa tutaendelea na utamaduni mbaya wa kuzifanya tofauti zetu za kisiasa kuwa ni chanzo cha uadui, chuki na hivyo kuhatarisha amani, utulivu na umoja wa taifa letu na watu wake.

Taarifa kutoka Ikulu, Dar es Salaam, tarehe 14/08/2007

__________

JK NA TAIFA STARS

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akitia sahihi kwenye mpira akiwa na rais wa TFF Leodgar Chilla Tenga alipotembelea kambi ya taifa stars katika hoteli ya Golden Tulip.

__________

Mheshimiwa Kikwete akipokea mpira ambao umesainiwa na wachezaji wote wa taifa stars. Anyempa mpira huo ni Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Serengeti, Mheshimiwa Jaji Bomani.

__________

Kikwete akichangamsha baraza kidogo kwa kuwapa moyo vijana wa taifa stars katika mechi yao ya kesho tarehe 08/09/2007, na timu ya taifa ya Msumbiji ambayo itafanyika Dar es salaam. JK aliwaambia vijana kuwa ana matumaini kuwa kesho vijana watashinda na ushindi utakuwa mtamu, lakini ya mungu mengi. Katika mazungumzo yake alisema kuwa yeye atakwenda Arusha kikazi lakini kama akimaliza mapema atarudi kuja kushangilia na rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume atakuwepo kuongoza mashabiki katika ushangiliaji.

__________

JK akipozi na timu ya taifa stars katika kuwapa moyo na mechi ya kesho na Msumbiji. JK akionyesha kujihusisha kwake katika maendeleo ya michezo nchini ambayo yeye mwenyewe ameyasisitiza. JK alipitia kambini hapo moja kwa moja alipotoka Kondoa katika ziara yake ya kikazi.

__________

Bango la kushabikia taifa stars likionekana waziwazi katika mitaa ya jijini Dar es salaam na pichani ni kaka Issa Michuzi akionyesha uzalendo wake katika pozi ya stamina kwa kusimama na mguu mmoja. Kaka uko fitiiiiii!


- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk