Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

TAREHE 08/09/2007

TAIFA STARS NA MSUMBIJI

Baada ya kungoja kwa hamu na kwa siku nyingi mechi ya mpira wa miguu baina ya taifa stars a na timu ya taifa ya Msumbiji, ile siku imefika (tarehe 08/09/2007). Mgeni wa heshima alikuwa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abedi Karume. Matokeo ni Tanzania 0 Msumbiji 1. Bado kuna kazi kubwa ya kufanywa.

__________

Matumaini yanaanza kuondoka baada ya kufungwa bao 1-0

__________

Washangiliaji wote wamekwisha nguvu baada ya kuona dakika za mwisho zinawadia na hakuna matarajio yoyote

__________

AJALI YA BASI - MBEYA

Basi la abiria la SABCO lililokuwa liktoka Tunduma kuelekea Dar es Salaam lilipata ajali na lori la kubebea mchanga lilipovaana uso kwa uso na kupoteza maisha ya watu zaidi ya watu 28 na kujeruhi zaidi ya watu 30. Ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Igurusi, wilaya ya Mbarali, Mbeya.

Katika ajali hiyo alikuwamo muimbaji maarufu Shenazi Salim (33) pichani chini, ambaye alikuwa akitokea Mbeya na basi la SABCO.

Shenazi kazikwa tarehe 11/09/2007

__________

Hili ndilo gari lililobeba mchanga lililogongana na basi la SABCO huko Mbeya

__________

Majeruhi

__________

Mmoja wa waliojeruhiwa akihojiwa na polisi ili wapate utambulisho wake


TAREHE 09/09/2007

MASHINDANO YA KUMENYA VIAZI

Mashindano ya kumenya viazi yaliyofanyika Mbeya katika uwanja wa Sokoine


TAREHE 10/09/2007

UZALENDO

Uzalendo


TAREHE 11/09/2007

BALOZI NCHINI UAE

Balozi wa Tanzania nchini U.A.E, Mheshimiwa Mohamed Maharage (mwenye tai nyekundu) alikuwamo katika mmoja wa mabalozi kumi walioalikwa rasmi katika mualiko aliouandaa Mfalme wa Abu dhabi, Sheikh Khalifa Bin Zayed Al Nahyan

__________

AJALI MJINI - DAR ES SALAAM

Ajali ya magari yaliyokwaruzana katika mtaa wa Samora na kusababisha msongamano wa magari, Dar es salaam


TAREHE 12/09/2007

KUKARIBISHA MWEZI MTUKUFU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Mheshimiwa Amani Abeid Karume akitoa hutuba ya kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhan huko ikulu ya Zanzibar


TAREHE 13/09/2007

MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN


TAREHE 14/09/2007

MLIMA WA KITONGA

Huu ndio mlima maarufu wa Kitonga nchini Tanzania. Kitonga unasemekana una kona 32 kama uzionavyo pichani mpaka kufika chini au kileleni. Kama dereva kazi kwako.


- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk