Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

TAREHE 15/09/2007

MHESHIMIWA MUDHIHIR MUDHIHIR

Mbunge wa Mchinga mheshimiwa Mudhihir Mudhihir alitembelewa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili mjini Dar es Salaam na waziri wa usalama wa raia mheshimiwa Harith Bakari Mwapachu. Mheshimiwa Mudhihir alilazwa hospitali ya Muhimbili baada ya kupata ajali ya gari huko mkoani Lindi ambayo ilisababisha akatwe mkono wake wa kulia.

__________

Mheshimiwa Jakaya Kikwete akimuapisha luteni jenerali Abdulrahman Shimbo kuwa Mnadhimu mkuu wa jeshi

__________

Mheshimiwa Jakaya Kikwete akimuapisha mkuu mpya wa majeshi jenerali Davies Mwamunyange


TAREHE 16/09/2007

SANAMU KARIBU NA LONDON BRIDGE

__________

__________

Sanamu la muogeleaji ambalo limeshindiliwa ardhini katika ufukwe wa kusini mwa mto Thames, London, karibu na daraja maarufu la 'London Bridge' ambalo tangu liwekwe limevutia wapita njia wengi wakiwamo wakazi na watalii wa London. Sanamu hilo limetayarishwa kutangaza kipindi maalum ambacho kitakuwa kinaonyeshwa katika kipindi cha Discovery Channel kila Jumapili, saa nne usiku kuanzia tarehe 23/09/2007.

__________

Sanamu lingine limewekwa katika 'concourse' ya Victoria station


TAREHE 17/09/2007

HESHIMA NI KITU CHA BURE

Mheshimiwa Augustine Mrema (pichani juu) akionekana akimpa mkono wa heshima rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete. Mbali na kuwa ni wapinzani wa vyama, lakini inadhihirisha kuwa tuna utamaduni mzuri wa kiungwana na wa kibinadamu ambao tumekuwa nao katika nchi yetu ya Tanzania.


TAREHE 18/09/2007

DAR ES SALAAM

Hili ni moja ya majengo yanayopendezesha Dar es Salaam hivi sasa

__________

AFANDE

kuwa afande inalipa samtaimu!


19/09/2007

NYANGUMI MJINI PAJE - ZANZIBAR

 

Wakazi wa kitongoji cha Paje, Zanzibar, wakijipatia rizki ya mafuta ya nyangumi ambaye alikutwa pembeni mwa bahari. Inasemekana, mafuta ya nyangumi ni dawa ya maradhi tofauti ambayo hutumika huko nyumbani.

__________

KAZI NI KAZI

Kumbuka! Kazi ni kazi tu popote pale ulipo!


20/09/2007

MATT DAMON NA BEN AFFLECK NDANI YA TANZANIA

Wasanii maarufu katika filamu za Hollywood, Matt Damon (kulia) na Ben Affleck (wa tatu kutoka kulia mwenye t-shirt nyeupe) walikuwa Tanzania katika matembezi yao ya kusaidia mayatima.

__________

21/09/2007

KITUO CHA MNAZI MMOJA

Kituo cha basi cha Mnazi Mmoja cha kubebea abiria haraka-haraka kionekanavyo hivi sasa.

__________

KATUNI

Cheka na vikatuni

__________

Hii sio katuni


- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk