Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

TAREHE 22/09/2007

HALI YA HEWA YACHAFUKA DUNIANI

Watu kumi na tano wamekufa kwa kuzama kwenye mafuriko yaliyoikumba Kenya na kuua watu mia mbili katika nchi tofauti za Afrika ambazo zimekumbwa na mafuriko hayo. Pichani juu, ni kijiji cha Budalangi, mashariki mwa Kenya.

__________

__________

UGANDA

__________

Uganda imepatwa na mafuriko na kuathiri makazi ya wananchi. Baadhi ya wakazi wakionekana wakivuka mto Aswa uliopo kaskazini mwa Uganda.

__________

SLOVENIA

__________

Slovenia pia imepatwa na mafuriko na inasemekana watu wanne wamekufa kwa kuzama na maji na wengine kupotea baada ya mafuriko kuyakumba mji wa Zelezniki ambao upo maili 30 kutoka mji mkuu wa Slovenia, Ljubljana. Slovenia haijawahi kupata mafuriko ya namna hiyo zaidi ya miaka thelathini.

__________

ENGLAND

__________

__________

__________

Baadhi ya sehemu za kusini na sehemu kanda ya kati ya England zilikumbwa na kimbunga cha nguvu ambacho kiliathiri makazi ya watu, magari na kuchimbua miti na mapaa ya nyumba.


TAREHE 23/09/2007

HOTELI YA SEA CLIFF DAR ES SALAAM YAUNGUA

__________

__________

__________

__________

Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Dar es Salaam, ambayo ilitengenezwa kiutamaduni na mapaa ya makuti, imeungua asilimia 75 ya makuti hayo na kuicha hoteli hiyo nyang'a nyang'a. Moto huo ambao unasemekana ulianzia aidha jikoni au chumba cha wafanyakazi, ulianza tangu saa kumi na mbili za jioni mpaka kufika kwa wana zima moto na kuutuliza moto huo kwenye mida ya usiku. Hakuna aliyejeruhiwa wala aliyekufa.


TAREHE 24/09/2007

SEA CLIFF HOTEL - HIVI LEO

__________

__________

__________

__________

__________

Hoteli ya Sea Cliff, baada ya kuungua sana!


TAREHE 25/09/2007

KIKWETE ASISITIZA MUUNGANO WA WATANZANIA POPOTE PALE WALIPO

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, mheshimiwa Jakaya Kikwete akizungumza na watanzania nane waliopo Marekani katika hoteli ya Grand Hyatt, New York. JK alizungumzia kuundwa chombo na jitihada za kuunganisha watanzania wote waliokuwapo nje na Tanzania

__________

KARIAKOO

Mtaa wa Swahili na Msimbazi, Kariakoo, Dar es Salaam, ionekanavyo hivi leo.


TAREHE 26/09/2007

TRAFIKI KAZINI

Trafik akionekana kujaribu kuzishtua-shtua taa za barabarani ambazo zilizokuwa zikileta mushkeli kidogo.

__________

DAR ES SALAAM SKYLINE

Sura ya Dar inaanza kubadilika na maendeleo yanashamiri.


27/09/2007

MHESHIMIWA KIKWETE AKIHUTUBIA KATIKA UMOJA WA MATAIFA

Rais wa Tanzania akihutubia umoja wa mataifa huko Marekani. Kwa ripoti kamili ya Mheshimiwa, dokoa hapa.


28/09/2007

TUJIKUMBUSHE ENZI HIZO

Huyo ni mshabiki wa Simba alikuwa akijitokeza na mbuzi zake kwenye mashindano makubwa ya wakati huo baina ya Simba na Yanga za Tanzania. Pichani ni uwanja wetu wa taifa ulivyokuwa zamani.

KARATE

Cheka na vikatuni


- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk