Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

TAREHE 29/09/2007

JOSEPH NA JOSEPHINE

__________

__________

__________

__________

__________

Joseph na Josephine walikuwa wachumba wa muda mrefu huko Marekani ambao waliwekeana ahadi ya kuwa pamoja maishani. Joseph alipata nafasi ya kupelekwa Iraq kupigana vita. Katika harakati za vita, kikundi cha Joseph kilipigwa bomu na Joseph alijeruhiwa na kuunguwa vibaya sana mwili mzima. Inavyosemekana, jinsi unavyomuona usoni ni afadhali kuliko maungo yake mengine ya ndani ya mavazi yake. Lakini pamoja na hayo yote, Josephine alikuwa tayari kuwa na mpenzi wake aliyeweka naye ahadi ya kuwa naye maishani milele na kukubali kufunga nae pingu za maisha. Ama kweli ahadi ni kitu kikubwa kwa yule anayeiweka moyoni.


TAREHE 30/09/2007

JELA YA AUSTRIA

__________

__________

__________

__________

__________

__________

__________

__________

__________

__________

__________

Picha za hapo juu ni za jela ya Austria


01/10/2007

URAIA WA NCHI MBILI

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, amesema serikali itahakikisha sheria ya uraia wa nchi mbili inapitishwa kwa manufaa ya Watanzania na taifa na si vinginevyo.

Akizungumza na baadhi ya Watanzania waliokutana naye mjini New York wiki iliyopita katika hoteli ya Grand Hyatt, Waziri Membe alisema lengo la serikali ni kuwasaidia Watanzania na si kugawa uraia wa Tanzania kwa wageni wenye uraia wa nchi zao.

Alisema haingii akilini ni kwa nini Mtanzania wa kuzaliwa anyang’anywe uraia wa Tanzania kwa kuwa amechukua uraia wa nchi nyingine kutafuta faida za kielimu, ajira au hata matibabu.

“Ni kwa nini tumuadhibu huyu Mtanzania wa kuzaliwa kwa kuwa tu amechukua uraia wa nchi nyingine ili apate elimu ama ajira na kusaidia ndugu zake waliobaki Tanzania?” alihoji Waziri Membe.

Waziri alisisitiza kuwa sheria hiyo itakapopitishwa haitatoa mwanya kwa kila mtu kuuvamia uraia wa Tanzania bali itawalinda Watanzania wanaotaka kuchukua uraia wa nchi za nje kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Akitoa mfano mmojawapo bila kutaja majina ya wahusika, Waziri Membe alisema anaifahamu familia moja ya Watanzania ambayo ililazimika kuchukua uraia wa Kanada kwa sababu za matibabu, na kwamba kuwanyang’anya uraia watu hawa ni kuwaadhibu bila kujali uhai wao.

Alieleza kuwa familia hiyo ina watoto wawili ambao matibabu yao hugharimu dola 2,000 kwa kila mmoja kwa mwezi, na kwamba kwa kuchukua uraia wa Kanada, matibabu hayo yanakuwa bure. Alihoji je, ni haki kuwanyang’anya uraia wao wa Tanzania?

Akitoa mfano wa manufaa yanayopatikana Ghana, Waziri Membe aliwaambia Watanzania hao kwamba ni muhimu kwa Tanzania kutumia raia wake walioko nje kwa manufaa ya taifa na siyo kuwabagua.

“Mwaka jana pekee wananchi wa Ghana walioko nje waliingiza dola bilioni 2.5 kwa njia mbalimbali halali,” na akaongeza: “Taifa dogo kama Komoro, mwaka jana lilipata dola milioni 89 kutoka kwa wananchi wake walioko Ufaransa pekee.

Akifafanua zaidi, Waziri Membe alisema wakati akiwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kipindi kisichofikia miaka miwili, Tanzania ilitoa uraia kwa wageni 101 na kushangaa ni kwa nini Watanzania wa kuzaliwa wapoteze uraia wao.

Waziri Membe aliwataka Watanzania kujenga umoja thabiti na kuwahakikishia kwamba serikali itakuwa pamoja nao ili kuleta maendeleo kwa taifa, na kwamba mawazo kuwa usalama wa taifa utakuwa hatarini si la jambo kuhofia iwapo sheria itatungwa vizuri.

Tanzania ina raia wake waliosambaa nchi mbalimbali duniani huku idadi kubwa ikiwa katika nchi za Kiarabu za Ghuba ambako wakati serikali ikiongeza ofisi moja ya Ubalozi nchini Oman miaka michache iliyopita ilikadiria kuwa kuna Watanzania laki tano.

Nchi nyingine ambazo Watanzania wanakadiriwa kuwa wengi ni za Marekani Kaskazini na Ulaya Magharibi ambako wako kwa maelfu, ambao wengi wao hukabiliwa pia na utata wa uraia wa watoto wao wanaozaliwa ugenini.

Mjadala wa suala la uraia wa nchi mbili umekuwa ukiendelea nchini katika siku za karibuni ambako kumeibuka kambi za wanaopinga kwa madai ya kulinda maslahi ya nchi na wanaounga mkono kwa madai hayo hayo ya kulinda maslahi ya nchi.

Habari na Mobhare Matinyi, New York.

__________

JK NDANI YA NEW YORK

Mheshimiwa Jakaya Kikwete akipokea mpira kutoka kwa mmoja wa watanzania wanaoishi Marekani.


02/10/2007

MLIMA WA KILIMANJARO

Mlima wetu wa Kilimanjaro uonekanavyo hivi sasa.

__________

DOKTA ALIPITIWA KIDOGO!

Daktari wa kienyeji alipitikiwa na usingizi kidogo alipokuwa kazini.

__________

MTAA WA SAMORA

Huu ni mtaa wa Samora Avenue uonekanavyo hivi sasa.

__________

BIG BEN YAVUMA TENA

__________

__________

__________

__________

__________

__________

__________

Saa maarufu duniani yenye kengele ya Big Ben ambayo ipo Westminster, imerudi tena ulingoni baada kufanyiwa matengenezo muhimu. Kengele hiyo iligonga kwa mara ya mwisho tarehe 11/08/2007 kwa matengenezo hayo ya karibu miezi miwili na kuanza kuwika tena katikati ya jiji la London. Mwaka 2009, Big Ben itasheherekea miaka 150 tangu ianze kazi yake. Kwa habari zaidi ya Big Ben, dokoa hapa.

__________

03/10/2007

UWANJA WA NDEGE - DAR ES SALAAM

Uwanja wetu wa ndege wa taifa uliopo Dar es Salaam.

__________

Uwanja wetu wa taifa ukiwa katika kumaliziwa na matengenezo madogo madogo.


04/10/2007

NEMBO MPYA YA AIR TANZANIA

Hio ni moja wa mfano wa nembo za ndege zetu mpya zitakavyokuwa. Air Tanzania wameagiza baadhi ya ndege kutoka Airbus (shirika la utengenezaji ndege) ili kutanua huduma zake.

__________

STESHENI

Kituo cha daladala cha stesheni kikionekana hivi sasa. Kwa mbali ni jengo la Kastam.


05/10/2007

MAENDELEO YA UWANJA WA KARUME

Uwanja wa Karume ukionekana umemwagiwa changa la kutiwa nyasi feki za kimataifa. Maendeleo hayo ni moja ya kuutengeneza na kuutayarisha uwanja wa Karume kwa mazoezi ya timu ya taifa na vijana.

__________

SKILLS

Kijana akionekana katika mitaa ya Dar es Salaam akionyesha utundu wake wa kuziruka baiskeli huku akiwa amevaa roller skates au (viatu vya magurudumu).

__________

ENZI ZAO!

Haidar Omar Abeid (Muchacho) ambaye alikuwa kepteni wa timu ya Simba akipokea kombe la ubingwa ambalo Simba walijinyakulia katika ligi kuu ya mwaka 1975. Haidar hivi sasa anaishi uarabuni.

__________

KATUNI ZA ZAMANI

Cheka na vikatuni.


- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk